About Us-nil

JIUNGE NASI

Sifa Za Kujiunga na Mapambazuko Saccos Ltd

Uwe mwajiriwa wa Taasisi ya umma au binafsi

Awe ametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea

Kujaza fomu ya uanachama

Kulipa kiingilio cha Sh. 83,000

Kuchangia akiba kila mwezi (kima cha chini 20,000)

Kulipa hisa kila mwezi (kima cha chini Sh. 10,000)

Kuchangia michango ya mwezi kupitia mshahara

Huduma zingine zitatolewa kwa kuzingatia vigezo na masharti ya huduma husika.

Uwe na kitambulisho cha NIDA

Picha 2 za rangi(passport size)

Haki Za Mwanachama Wa Mapambazuko Saccos Ltd

  • Kushiriki kikamilifu katika shughuli za Chama ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mikutano yote inayohusika;
  • Kushiriki katika kutoa uamuzi wa mambo mbalimbali katika Mikutano Mikuu;
  • Kupiga kura chini ya misingi ya mtu mmoja kura moja bila kujali idadi ya Hisa anazomiliki;
  • Kuchagua na/au kuchaguliwa katika Uongozi wa chama.
  • Kuwa na haki sawa kuhusu mali ya Chama na kudhibiti ipasavyo matumizi yake;
  • Kupatiwa huduma zozote zinazotolewa na chama ilimradi amekidhi masharti yanayoambatana na huduma hiyo;
  • Kupatiwa taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za Bandarini SACCOS, muhtasari wa mkutano na nyaraka nyingine za chama kwa ajili ya mapitio akiwa katika ofisi za chama;
  • Kuteua Mrithi;
  • Kupokea gawio na faida nyingine kutoka katika shughuli za chama kwa kuzingatia masharti.