Mikopo ya Dharura

Mikopo ya dharura itatolewa kwa wanachama kwa  ajili ya kukidhi mahitaji yao ya dharura .

  • Mwanachama atajaza fomu ikionyesha lengo na kiasi cha mkopo,kamati ya mikopo itaidhinisha mkopo huo pindi tu kanuni zote zitakapotekelezwa.
  • Kiwango cha juu cha mkopo huu ni Tsh. 3,000,000/=.
  • Muda wa marejesho hautazidi miezi 12.
  • Mkopo utakaotolewa hautazidi akiba za mwanachama alizonazo.
  • Dhamana kwa  mikopo ya dharura itakuwa akiba alizonazo mwanachama.
  • Riba itategemea sera ya bei ya wakati husika . Kwa sasa ni 3% kwa mwezi.
  • Mikopo ya dharura itatolewa wakati wowote alimradi pawepo na fedha katika Chama.
  • Mwanachama anaweza kukopa mkopo wa dharura hata kama ana mikopo mingine(kama vile Mkopo wa maendeleo,  papo kwa papo au elimu). Itategemea  urejeshaji wake mzuri.