Mikopo ya Elimu

  • Kiwango cha juu cha mkopo wa elimu kitakuwa ni Shs 2,000,000/=
  • Mkopaji ataweza kukopa sio zaidi ya akiba zake Chamani.
  • Mkopaji atakopeshwa kwa kuzingatia kigezo cha theluthi moja ya akiba kwa jumla ya mikopo yote.
  • Mwanachama atajaza fomu maalum ya mkopo wa elimu
  • Kamati ya mikopo itajadili ikiridhika itaidhinisha mkopo huo pasipo kuchelewa
  • Maelezo ya kujitosheleza kuhusu shule/chuo jina la mwanafunzi yatahitajika
  • Mwanachama atakopa kwa lengo la elimu tu na si vinginevyo
  • Muda wa juu wa kurejesha mkopo wa elimu ni miezi sita.
  • NB; Mkopo huu, kama ilivyo mikopo mingine, utaanza kurejeshwa mwezi unaofuata baada ya mkopo kuchukuliwa.