Mikopo ya Maendeleo

Mikopo itatolewa kwa wanachama waliokidhi masharti na taratibu za mikopo.

 • kiwango cha juu cha kukopa kwa sasa ni 40,000,000.00/=
 • Mwanachama atakayekopa mkopo huu, chini ya Tsh 3,000,000/=, atapaswa kuurejesha ndani ya miaka miwili.
 • Mikopo ya maendeleo itatolewa kwa awamu kwa kufuata vikomo vifuatavyo:
  • Mkopo wa kwanza shs.5,000,000/= hadi 10,000,000/=
  • Mkopo wa pili kuanzia shs 10,000,000/= hadi 20,000,000/=
  • Mkopo wa tatu hadi shs 20,000,000/=
  • Mkopo wa nne hadi shs 30,000,000/=
  • Mkopo wa tano hadi shs 40,000,000/=.
  • Kila kikomo lazima kipitiwe na mkopaji ndipo aweze kupewa mkopo wa juu zaidi. Mwanachama ambaye atakuwa analipa marejesho yake kikamilifu kupitia makato ya mshahara ataruka kikomo kimoja baada ya kingine.
 • Mkopaji ni lazima alete barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa ya ukaazi wa mahali anapoishi kwa sasa.
 • Muda wa mkopo hautazidi miezi 36.
 • Riba ya mkopo itaendana na hali ya soko. Kwa sasa ni 1.7%  kwa mwezi.
 • Mkopaji atalipia bima mkopo wake kabla ya kupewa hundi yake kulingana na bei ya soko (kwa sasa ni 0.9% kwa mkopo usiozidi mwaka mmoja na 1.4% kwa mkopo unaozidi mwaka mmoja katika marejesho).
 • Mkopaji lazima awe na akiba inayomwezesha kukopa mara tatu kwa kiwango cha juu. (Mwanachama anayetaka kukopa zaidi ya mkopo mmoja kwa wakati mmoja , jumla ya mikopo yote  lazima izingatie kigezo cha kuwa na theluthi moja ya akiba  Chamani).
 • Mwenzi wa mkopaji lazima ashiriki kwa kuandika barua/affidavit yenye picha yake ya kuridhia mali yao kuwekwa dhamana na pia kuwepo uthibitisho wa kisheria kuwa huyo ni mume/mke wa mkopaji.  Afisa mikopo lazima ajiridhishe  kuwa mwenza wa mkopaji ndiye mwenye picha iliyobandikwa  kwenye barua/affidavit na  ndiye aliyeweka saini na dole gumba panapohusika.
 • Ikiwa mkopaji hana mke/mume aandike hati ya kiapo (affidavit) ya kuthibitisha kuwa hana mke/mume na ihakikiwe na Afisa mikopo.
 • Iwapo fedha hazipo za kutosha na fomu za mikopo zimeidhinishwa na kamati ya mikopo , mikopo midogo italipwa kwanza ndipo ifuate mikopo mikubwa. Mikopo mikubwa ambayo itakuwa haijalipwa awamu ya kwanza ndiyo itakayoanza kulipwa awamu inayofuata.