Mikopo ya Papo kwa Papo

  • Kiwango cha juu kwa mkopo wa papo kwa papo kitabaki kuwa Tshs 200,000/= .
  • Mkopo wa papo utatolewa kwa mwanachama kwa ajili ya kukidhi mahitaji yake ya haraka.
  • Mwanachama atajaza fomu maalum iliyoandaliwa kwa ajili hiyo.
  • Muda wa mkopo hautazidi siku 30.
  • Dhamana ya mkopo itakuwa akiba za mwanachama.
  • Riba itategemea sera ya bei ya wakati husika(riba ya sasa ni 5% kwa mwezi)
  • Hutolewa wakati wowote ali mradi pawepo na fedha katika hama.
  • Adhabu itakuwa 2.5% kwa kila juma (10% kwa mwezi) ya mkopo uliolala.
  • Iwapo siku ya 30 itaangukia kwenye mapumziko mkopo utalipwa siku inayofuata ya kazi.