“Ningependa kutoa shukrani zangu kwa Mapambazuko Saccos kwa kunipa nafasi ya kupata mkopo ulioniwezesha kupanua biashara yangu ya kuuza nafaka. Mchakato wa kupata mkopo ulikuwa rahisi na wa haraka, na huduma nilizopata zilikuwa za kitaalamu sana. Kwa sasa nimeweza kuongeza bidhaa, wateja wameongezeka, na maisha yangu yamebadilika.”