From MWANANCHI

Kumbuka huwezi kuwa mfanyabiashara mkubwa na maarufu bila kukopa. Kama unaogopa kukopa basi sahau ndoto ya kuwa mfanyabiashara mkubwa. Hiyo ni nukuu ya Reginald Mengi, mfanyabiashara mashuhuri aliyefariki juzi.

Kama ilivyo maana ya mkopo kwa tafsiri rahisi ni makubaliano ya kupeana fedha au vitu kwa lengo la kurudisha baada ya muda mliokubaliana.

Mikopo mingi huwa na riba kwa sababu wakopeshaji ni wafanyabiashara, inaweza kuwa na dhamana au siwe nayo kulingana na makubaliano, ingawa mingi uhitaji dhamana.

Ukitumiwa vizuri unaweza kuongeza ufanisi wa kibiashara, kupanua wigo na hata kuzaa mafanikio chanya, pia huwasaidia wafanyabiashara kuwa na nidhamu ya fedha kwa sababu wataishi wakijua wanatakiwa kuurudisha.

Kama ilivyo ada duniani kila lenye faida lina hasara zake, na mikopo vivyo hivyo ina faida ambazo baadhi nimezitaja na ina hasara.

Kwa bahati mbaya hasara za mikopo huendana na fedheha, kudhalilika na hata kukuhamisha eneo moja kwenda lingine.