Mikopo ya Elimu
Home / Mikopo ya Elimu
- Kiwango cha juu cha mkopo wa elimu kitakuwa ni Shs 2,000,000/=
- Mkopaji ataweza kukopa sio zaidi ya akiba zake Chamani.
- Mkopaji atakopeshwa kwa kuzingatia kigezo cha theluthi moja ya akiba kwa jumla ya mikopo yote.
- Mwanachama atajaza fomu maalum ya mkopo wa elimu
- Kamati ya mikopo itajadili ikiridhika itaidhinisha mkopo huo pasipo kuchelewa
- Maelezo ya kujitosheleza kuhusu shule/chuo jina la mwanafunzi yatahitajika
- Mwanachama atakopa kwa lengo la elimu tu na si vinginevyo
- Muda wa juu wa kurejesha mkopo wa elimu ni miezi sita.
- NB; Mkopo huu, kama ilivyo mikopo mingine, utaanza kurejeshwa mwezi unaofuata baada ya mkopo kuchukuliwa.